4.0 KISWAHILI (102)
4.1 MATOKEO YA MTIHANI WA SOMO LA KISWAIIILI MWAKA WA 2010
Jedwali hili Iinaonyesha matokeo ya mtihani wa somo la Kiswahili katika muda wa miaka minne (2007 hadi 2010).
Jedwali 4: Matokeo ya mtihani wa Kiswahili (2007 – 2010)
Mwaka | Karatasi | Watahiniwa | Alama ya Juu | Alama ya Wastani | Alama ya Tanganisho |
2007 | 1 2 3 Jumla | 272,905 | 40 80 80 200 | 15.80 32.22 43.49 91.51 | 6.42 11.91 13.12 27.00 |
2008 | 1 2 3 Jumla | 304,314 | 40 80 80 200 | 14.20 29.18 31.17 74.55 | 7.18 11.43 13.64 32.25 |
2009 | 1 2 3 Jumla | 335,377 | 40 80 80 200 | 15.40 29.03 32.72 77.15 | 6.93 11.96 13.11 32.00 |
2010 | 1 2 3 Jumla | 354,738 | 40 80 80 200 | 14.32 33.77 39.22 87.10 | 6.53 11.96 14.09 28.73 |
Jedwali hili laonyesha kuwa kwa ujumla:
Alama ya wastani ya karatasi ya 1(102/1) ya mwaka wa 2010 imeshuka ikilinganishwa na mwaka wa 2009.
Matokeo ya karatasi ya pili (102/2) ya mwaka wa 2010 yameshuka yakilinganishwa na yale ya mwaka wa 2009.
Matokeo ya karatasi ya tatu (102/3) ya mwaka wa 2010 yameimarika kutoka alama ya wastani 32.72 mwaka wa 2009 hadi 39.22 mwaka wa 2010.
Matokeo ya Kiswahili kama somo kwajumla katika mwaka wa 2010 yameimarika. Alama ya wastani ya Kiswahili kama somo mwaka huu ni 87.10 yakilinganishwa na mwaka wa 2009 ambapo alama hii ilikuwa 77.15(ongezeko la 10.16)
Alama ya tanganisho inaonyesha kuwa kuna baadhi ya watahiniwa ambao waliweza kujipatia alama nyingi zaidi ya alama ya wastani mwaka wa 2010, ikilinganishwa na mwaka 2009. Alama hii ilikuwa 32.58.
INSHA (102/1)
Jedwali 5: Matokeo ya Karatasi ya kwanza ya miaka ya 2007 – 2010.
Mwaka | 2007 | 2008 | 2009 | 2010 |
Alama ya Wastani | 15.80 | 14.20 | 15.40 | 14.32 |
Alama ya Tanganisho | 6.42 | 7.18 | 6.93 | 6.53 |
Jedwali hili laonyesha kwamba kwa miaka hii minne (2007-2010), matokeo ya karatasi ya 102/1 yamekuwa yakipanda na kuteremka na kwamba watahiniwa wengi hawajaweza kujipatia alama zaidi ya nusu ya alama zote ambazo zinaweza kutuzwa ambazo ni 40. Katika mwaka wa 2010, matokeo haya yaliteremka kwa kiasi cha alama 1.08.
Kiswahili Form 1
Kuandika
Kusikiliza na Kuzungumza
Kusoma
Sarufi Na Matumizi ya Lugha
Kiswahili Form 2
Kuandika
Kusikiliza na Kuzungumza
Kusoma
Sarufi Na Matumizi ya Lugha
Kiswahili Form 3
Kuandika
Kusikiliza na kuzungumza
Kusoma
Sarufi na Matumizi ya Lugha
Kiswahili Form 4
Kuandika
Kusikiliza na Kuzungumza
Kusoma kwa Mapana
Sarufi na matumizi ya Lugha